0%
Skip to main content

Vifaranga wanahitaji uangalizi mkubwa sana hasa katika hatua za mwanzo za ukuaji wao, na moja ya njia zinazoweza kuhakikisha usalama wa maisha yao kwanza wao kwa wao (yaani vifaranga) na usalama wa mayai hapo baadaye ni kwa kuwakata midomo.  

Zoezi hili hufanyika pia kwa lengo la kusaidia kuzuia upotevu wa chakula kutokana namna vifaranga wanavyodonoa donoa chakula wakati wa kula. Mara nyingi huwa wanakitawanya chakula vibaya kutokana na urefu wa midomo yao. Hivyo wanapofikisha umri wa siku 7-10 zoezi hili la kuwapunguza midomo  hufanyika  kisha kurudiwa tena  wanapokuwa na umri wa kati ya wiki 8 hadi 10  

Vifaa maalum hutumika kukamilisha zoezi hili, na kwa anayefuga kitaalam ni vema zoezi hili likafanywa na mtaalam kwa kuwa linahitaji umakini wa hali ya juu ili vifaranga wasidhurike macho wala ulimi.  Mtaalam atachunguza kwanza makali na joto la wembe wa kifaa cha kukatia midomo kabla ya kuanza zoezi. Kisha ataanza kukata mdomo mmoja baada ya mwingine yaani wa juu kisha wa chini ama vinginevyo.  

Jukumu kwa mfugaji ni kuhakikisha kuwa joto la mazingira sio kali sana, vifaranga wana afya njema na wamepatiwa vitamini kabla ya kuanza zoezi la ukataji midomo na mara baada ya zoezi kukamilika hakikisha kuku wanapatiwa chakula cha kutosha na maji yenye vitamin wakati wote kwa muda wa wiki nzima.  

Leave a Reply