Interchick wamefungua kituo cha huduma za mifugo ambapo uchunguzi wa kimaabara ili kutambua vyanzo vya magojwa kwa kuku hufanyika.
Watu wengi inawezekana wamekuwa wakijiuliza kwamba kituo cha mifugo kilichofunguliwa na Interchick ni kwa ajili ya wafugaji wa Interchick pekee? La hasha! kituo ni kwa ajili ya wafugaji wote wa kuku, yeyote mwenye uwezo wa kufika kituoni hapo basi atapatiwa huduma stahiki.
Ambapo mbali na mfugaji kupewa ushauri wa kitaalam kuhusu kuzifahamu dalili za magonjwa kwa mifugo, kituo kinapokea sampuli na kuzipeleka maabara kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kujua kwa usahihi nini kinasumbua mifugo.
Utafiti unaonyesha kuwa kwa Tanzania magonjwa yanayosumbua sana mifugo ya kuku ni kideri, gumboro, ndui na mareks. Wataalam wanaendelea kuwasisitiza wafugaji kutumia chanjo husika kwa wakati sahihi kwa ajili ya kuikinga mifugo yao na magonjwa hayo.
Kituo kina uwezo wa kupima na kubaini kiwango cha kinga kilichomo ndani ya mifugo kama kimefikia kiwango kinachohitajika kutokana na chanjo waliyochanjwa na kutoa ushauri
Katika kuiunga serikali mkono kwenye suala la kuhamasisha ulaji wa nyama nchini, Interchick ina mpango wa kuongeza wigo hapo baadae ili kuhudumia mifugo mingine kama ng’ombe na kadhalika ili kuboresha sekta ya ufugaji na kuhakikisha watanzania wengi wananufaika.